Exodus 4:24-26

24 aMusa alipokuwa mahali pa kulala wageni akiwa njiani kurudi Misri, Bwana akakutana naye, akataka kumuua. 25 bLakini Sipora akachukua jiwe gumu, akakata govi la mwanawe na kugusa nalo miguu ya Musa. Sipora akasema, “Hakika wewe ni bwana arusi wa damu kwangu.” 26Sipora alipomwita Musa, “Bwana arusi wa damu,” alikuwa anamaanisha ile tohara. Baada ya hayo Bwana akamwacha.

Copyright information for SwhKC